728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, December 04, 2015

    ARSENAL YARAHISISHIWA KAZI KUMSAJILI BENDER

    London,England.


    Klabu ya Arsenal imepata matumaini ya kumsajili kiungo wa ulinzi Mjerumani Lars Bender baada ya klabu yake ya Bayer Leverkusen kupitia kwa mwenyekiti wake Michael Schade kusema kuwa nyota huyo anaweza kuuzwa hapo mwezi januari mwakani.

    Bender,26 amekuwa akiwindwa kwa miaka mingi na Arsenal lakini safari hii ameonekana kuhitajika zaidi baada ya Arsenal kukumbwa na majeruhi wengi katika safu yake ya kiungo.Arsenal inamuona Bender kama mbadala sahihi wa kiungo wake Francis Coquelin ambaye yuko nje ya dimba baada ya kuumia goti katika mchezo ulioisha kwa Arsenal kulazimishwa sare ya 1-1 na Westbrom.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL YARAHISISHIWA KAZI KUMSAJILI BENDER Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top