Tunis,Tunisia.
Esperance imeamka kutoka katika usingizi wa kuchapwa magoli 3-0 na Etoile du Sahel wikendi iliyopita baada ya jana jumapili ikiwa nyumbani Olympique d'El Menzah kuitandika CS Sfaxien kwa magoli 2-1.
Esperance ilipata magoli yake dakika za 3 na 51 kupitia kwa Chamseddine Dhaouadi na Fekhredine ben Youssef huku Ali Maaloul akiifungia CS Sfaxien goli la kufutia machozi dakika ya 9.
Kufuatia ushindi huo Esperance imefanikiwa kufikisha jumla ya pointi 33, pointi moja chini ya vinara Etoile du Sahel wenye pointi 34 huku nafasi ya tatu ikishikwa na CS Sfaxien yenye pointi 28 na kufuatiwa na Metlaoui pamoja na CA Berzetin zenye pointi 20 kila moja.
0 comments:
Post a Comment