Madrid,Hispania.
Kura zilizoendeshwa na gazeti maarufu la michezo la Hispania la AS lenye makao makuu yake katika jiji la Madrid zimeonyesha kuwa mashabiki wa Real Madrid wanataka Zinedine Zidane ndiye awe kocha wa miamba hiyo na wala siyo Jose Mourinho ama Rafa Benitez.
AS liliwataka mashabiki hao wa "Los Blancos" kuyapigia kura majina hayo matatu na majibu yakawa hivi:
Kati ya kura 22,000 zilizopigwa na mashabiki hao, kura 11,600 zimemchagua Zidane,ambazo ni sawa na asilimia 52 ya kura zote.Jose
Mourinho amepata kura 7,300 ambazo ni sawa na asilimia 33 huku kocha wa sasa Rafa Benitez akiburuza mkia baada ya kuambulia kura 3,100 ambazo ni sawa na asilimia 14 ya kura zote.
Licha ya mashabiki kumtaka Zidane awe kocha mpya wa klabu hiyo baadhi ya wakurugenzi wa bodi ya Real Madrid wanaona Zidane bado hajaiva vya kutosha kuiongoza miamba hiyo ya ligi ya La Liga hivyo Perez anapaswa kuendelea kusaka kocha mwenye uzoefu zaidi.
Makocha wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya Benitez ikiwa atafukuzwa no Fabio Capello,Victor Fernandez na Joachim Law
0 comments:
Post a Comment