BADO NIPO!!Kama unadhani Kocha Jose Mourinho ana mpango wa kuondoka Chelsea hivi karibuni basi sahau,jamaa kasema bado anatamani kuendelea kuwa kocha wa matajiri hao wa London hata kwa miaka 10 zaidi.
Mourinho ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na mpango wa kutaka kurudi Real Madrid baada ya mambo kuendelea kumuendea kombo katika klabu ya Chelsea kiasi cha kupoteza matumaini ya kumaliza ligi katika nafasi nne za juu amesema bado anapenda kubaki klabuni hapo kwa kipindi kirefu zaidi.
Amesema "Kama Chelsea watanipa mkataba wa miaka 10,nitasaini mara moja.Unapokuwa na mkataba kwa hali ya kawaida unatamani kuumaliza na siyo kuuvunja.Alimaliza Mourinho ambaye usiku wa leo ana kibarua kigumu pale Chelsea itakapovaana na Leceister City katika mchezo wa ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment