Habari na Paul Manjale.
Muto:Klabu ya Manchester United inataka kuiongezea makali safu yake ya ushambuliaji hapo mwezi januari kwa kumsajili mshambuliaji wa Mainz ya Ujerumani Mjapan Yoshinori Muto mwenye thamani ya £10m.Msimu huu Muto,23 amefunga magoli 7 katika michezo 14 katika ligi ya Bundesliga huku kikosi kizima cha Manchester United kikifunga magoli 22 katika michezo 17.(The Mirror)
Krychowiak:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kutenga dau la £33m ili kujaribu kumsajili kiungo mkabaji wa Sevilla Mpolandi Grzegorz Krychowiak,25.(Sun)
Arteta:Arsenal haitampa tena mkataba mpya kiungo na nahodha wake Muhispania Mikel Arteta na badala yake nyota huyo anayesifika kwa uongozi mzuri nje na ndani ya uwanja atapewa nafasi ya kuwa mmoja kati ya makocha wa klabu hiyo ya London.Kwa kuanzia Arteta,34 ataanza na kikosi cha vijana cha Arsenal kabla ya kupandishwa mpaka kikosi cha wakubwa.
.
Vardy:Licha ya kuwa na mkataba mpaka mwaka 2018, Klabu ya Leicester City imepanga kumuongezea mshahara mara mbili zaidi mshambuliaji wake Jamie Vardy kutoka £40,000 mpaka £100,000 kwa wiki ili kuzima mpango wa kufikiria kuhama baada ya kuanza kumezewa mate na vilabu vya Manchester United,Chelsea na Tottenham.(The Mirror)
Mignolet:Mlinda mlango Simon Mignolet anatarajiwa kupewa mkataba wa miaka mitano na Liverpool utakaomuwezesha kupata mshahara wa £60,000 kwa wiki.(The Sun)
Jese:Liverpool imeripotiwa kuanza mikakati ya kutaka kumsajili mshambuliaji asiye na furaha katika klabu ya Real Madrid Jese Rodriguez,22.(Don Balon/Squawka)
0 comments:
Post a Comment