728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, December 22, 2015

    ZAMALEK YAFYATA MKIA YAAMUA KUENDELEA NA LIGI KUU

    CAIRO,MISRI.

    Mabingwa wa soka nchini Misri Zamalek FC wamebadilisha uamuzi wao wa kujiondoa katika ligi kuu ya soka nchini humo.

    Zamalek mwishoni mwa juma, walitangaza hatua hiyo baada ya kufungwa na klabu ya El-Gaish mabao 3 kwa 2 mchuano ambao wanasema mwamuzi wa mchezo huo
    aliwaonea.

    Uongozi wa klabu hiyo ulikutana siku ya Jumatatu na kubadilisha uamuzi huo kutokana na adhabu ambayo ilikuwa inawasubiri ikiwa wangeendelea na uamuzi huo.

    Ikiwa Zamalek ikiendelea na mpango wake,Shirikisho la soka nchini Misri lingeipiga
    marufuku ya mwaka mmoja klabu hiyo na kuishusha daraja.

    Aidha, mabadiliko hayo yamefanyika baada ya
    mashabiki wa Zamalek kusema ni vema wasijiondoe kwa sababu ni mwaka jana tu
    waliposhinda taji la soka nchini humo baada ya muda mrefu.

    Viongozi wa Zamalek wameamua kuliandikia
    Shirikisho la soka nchini humo kulalamikia namna mchuano dhidi ya El-Gaish ulivyochezeshwa na refarii Mahmoud Al Banna.

    Al Banna alimpa beki wa Zamalek Ali Gabr kadi nyekundu katika dakika za mwanzo za mchezo huo na kuwapa wapinzani wake
    penalti mbili, hatua iliyowakasirishaviongozi wa Zamalek.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ZAMALEK YAFYATA MKIA YAAMUA KUENDELEA NA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top