728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, December 22, 2015

    SAFARI YA MOURINHO MAN UNITED YAWIVA KINACHOSUBIRIWA NI MUDA TU

    Manchester, England.

    Ndoto ya Jose Mourinho kuifundisha Manchester United huenda ikatimia hivi karibuni baada ya vyombo mbalimbali vya habari vya England kudai kuwa tayari kocha huyo ameshafikia makubaliano ya awali na klabu hiyo na ndiye atakayerithi mikoba ya Louis Van Gaal pindi atakapotimuliwa kibarua chake.

    Taarifa zinadai kuwa mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward ameshakutana na Mourinho kuweka mambo sawa na kinachosubiriwa sasa ni wamiliki wa klabu hiyo familia ya Glazer kuamua ni lini watamtimua Van Gaal.

    Mourinho,56 ameendelea kukitaka kwa udi na uvumba kibarua cha kuinoa Manchester United licha ya kutoswa mwaka 2013 na nafasi hiyo kupewa David Moyes ambaye hakumaliza hata mwaka akatimuliwa baada ya timu kupoteza muelekeo na hata kushindwa kuingia nne bora.

    Taarifa zisizo rasmi sana zinadai ili kuonyesha kuwa amepania kutua Manchester United Mourinho yuko tayari kushusha mshahara toka £10m alizokuwa akilipwa Chelsea kwa mwaka mpaka £6m kwa mwaka.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAFARI YA MOURINHO MAN UNITED YAWIVA KINACHOSUBIRIWA NI MUDA TU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top