Cairo,Misri.
Mshambuliaji aliyewahi kutamba miaka ya nyuma kwa kufunga magoli alivyojisikia Mmisri Amr Zaki ‘The Bulldozer’ ambaye kwasasa amestaafu soka ameripotiwa leo hii kuwa yuko tayari kurejea tena dimbani ikiwa atapata ofa nono toka klabu yoyote ile.
Zaki ambaye alitangaza kuachana na soka mwezi Agosti baada ya kutemwa na klabu ya Arab Contractors amedai bado yuko fiti kufanya chochote uwanjani licha ya kuwa nje kwa muda mrefu sasa.
Kabla ya kutua Arab Contractors,Zaki aliwahi kukipiga na vilabu vya EIPPN,Zamalek na Wigan ya England huku akiisaidia Misri kutwaa vikombe viwili vya AFCON mwaka 2006 na 2008 na kufunga jumla ya magoli 29 katika michezo 63.
0 comments:
Post a Comment