728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 24, 2015

    ZAMALEK YAREJEA KWA KISHINDO LIGI KUU MISRI,YAIPIGA EL MAHALLAH 5-0

    CAIRO,MISRI.

    Baada ya kufuata mpango wake wa kususia ligi kuu ya Misri kwa madai ya kuonewa na waamuzi klabu ya Zamalek jana jumatano ilirejea kwa kishindo katika ligi hiyo kwa kuibamiza klabu ya Ghazl El-Mahallah kwa mabao 5-0 katika mchezo wa raundi ya 10.

    Mabao yaliyoipa ushindi huo mnono Zamalek yamefungwa na:Moustafa Kalusha (og) 31,
    Ahmed Mekki 33, 42,Mahmoud Kahraba
    54 na Mohamed Koffi 84.

    Kufuatia ushindi huo Zamalek imechupa mpaka nafasi ya 4 ikiwa na pointi zake 16 huku Ghazl el-Mahalla ikiburuza mkia baada ya kujikusanyia pointi 3 katika michezo 10.

    Vikosi 

    Zamalek: Ahmed El-Shennawy, Omar Gaber, Ahmed Dweidar, Mohamed Koffi,Hamada Tolba, Ibrahim Salah, Tarek Hamed, Ayman Hefni (Moustafa Fathi 60),
    Ahmed Hamoudi, Mahmoud Kahraba (Maarouf Youssof 68), Ahmed Mekki (Bassem Morsi 73)

    Ghazl El-Mahallah: Mohamad Fawzi,Khaled Abdel-Razek, Moustafa Kalusha,Ahmed El-Sissi (Hamed Faisal 46), Khaled Abdel-Razek,Mohamed Mohsen (Walid
    Nabil 89), Hossam Ghaly, Ahmed Abdel-All, Khaled El-Ekhmimi (Mohamed Yehya),
    Eslam Gamal, Ramadan Rabie.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ZAMALEK YAREJEA KWA KISHINDO LIGI KUU MISRI,YAIPIGA EL MAHALLAH 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top