Liverpool,England.
Leiceister City imeendelea kujichimbia kileleni mwa ligi kuu nchini England baada ya leo jioni kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Everton katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Goodison Park.
Magoli yaliyoipa ushindi Leceister City siku ya leo yamefungwa na Riyad Mahrez aliyefunga kwa mikwaju ya penati dakika za 27 na 65 pamoja na Shinji Okazaki dakika ya 69 huku Everton wakipata magoli yao kupitia kwa Romelu Lukaku na Kevin Mirallas dakika za 32 na 89.
Kufuatia ushindi huo Leceister City imefanikiwa kubaki kileleni mwa ligi kuu baada ya kufikisha pointi 38 ikifuatiwa na Arsenal yenye pointi 33 baada ya kucheza michezo 16.
Katika mchezo mwingine uliopigwa huko Stamford blidge magoli ya Branslav Ivanovic,Pedro Rodriguez yameipa Chelsea ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Sunderland.
Kutoka Manchester: Norwich City imeishusha Manchester United toka nafasi ya nne mpaka ya tano katika msimamo ya ligi kuu baada ya kuitandika kwa mabao 2-1.
Mabao yaliyoipa ushindi huo wa kihistoria Norwich City yamefungwa na Cameron Jerome pamoja na Alexander Tettey huku Antony Martial ikiifungia Manchester United goli la kufutia machozi.
Matokeo mengine ya ligi kuu yako kama ifuatavyo....
Southampton 0-2 Tottenham
Stoke City 1-2 Crystal Palace
Bournemouth 2-1 Westbrom
0 comments:
Post a Comment