728x90 AdSpace

Thursday, December 17, 2015

HATIMAYE GARRY NEVILLE APATA USHINDI WA KWANZA VALENCIA

Valencia,Hispania.

Baada ya kupata kichapo toka kwa Lyon katika michuano ya ligi ya mabingwa kisha sare dhidi ya Eibar katika ligi ya La Liga wikendi iliyopita hatimaye kocha Garry Neville amefanikiwa kupata ushindi wa kwanza akiwa na klabu yake ya Valencia.

Ushindi huo umepatikana baada ya Valencia kuitandika Barakaldo kwa mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano wa kombe la Copa del Rey uliopigwa katika dimba la Estadio Mestalla.

Magoli yaliyoipa ushindi Valencia na kuipeleka hatua ya 32 bora yamepatikana dakika ya 30 kupitia kwa Alvaro Negredo na dakika ya 9 kupitia kwa Santi Mina na kufanya Valencia wawe mafuzu kwa jumla ya magoli 6-1.

Matokeo mengine ya Copa de Rey

Getafe 3-1 Rayo Vallecano, Mirandes 1-0 Malaga, 
Athletic Bilbao 6-0 Real Balompedica


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: HATIMAYE GARRY NEVILLE APATA USHINDI WA KWANZA VALENCIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown