728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 17, 2015

    NYOTA LA LIGA AJA JUU BAADA YA KUDAIWA SHOGA

    Mexico.


                                                        Jonathan enzi akiwa FC Barcelona

    Nyota wa soka Jonathan Dos Santos amepinga taarifa zinazodai kuwa yeye ni shoga baada ya ripoti kutoka vyombo vya habari vya nchini kwao Mexico kudai kuwa nyota huyo ana mahusiano yasiyofaa na mchezaji mwenzake katika klabu ya Villarreal Matteo Musacchio.

    Taarifa kutoka gazeti la Mexico liitwalo TVNotaz zimedai kuwa Jonathan amekuwa na uhusiano huo mchafu na mlinzi wa Kiargentina Musacchio na hata kaka yake Giovan Dos Santos aliyewakukipiga FC Barcelona na Tottenham analijua suala hilo na amekuwa akimuunga mkono.



                                                                 Matteo Musacchio

    Jonathan amejibu tuhuma hizo kupitia ukurasa wake wa twitter kwa kusema "Kama ningekuwa shoga nisingeficha ningesema hadharani ili kila mtu afahamu.Tungeni vitu vingine.Msichochee ubaguzi na unyanyapaa.Alimaliza Jonathan ambaye kabla ya kutua Villarreal alipitia FC Barcelona.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NYOTA LA LIGA AJA JUU BAADA YA KUDAIWA SHOGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top