728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, December 16, 2015

    KOMBE LA DUNIA LA VILABU:SAMATTA NA TP MAZEMBE YAKE DIMBANI TENA LEO

    Osaka,Japan.

    Klabu ya TP Mazembe ya Congo inayochezewa na Watanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu leo jumatano saa 10:30 itashuka dimbani huko Nagai,Osaka kuvaana na Club America ya Mexico katika mchezo wa kusaka mshindi wa tano na sita wa michuano ya vilabu bingwa duniani inayoendelea nchini Japan.

    TP Mazembe na Club America zinaingia dimbani kusaka ushindi wa tano/sita baada ya kupoteza michezo yao ya robo fainali iliyopigwa wiki iliyopita.

    TP Mazembe ilifungwa na wenyeji Sanfrecce Hiroshima kwa mabao 3-0 huku Club America yenyewe ikifungwa na Guangzhou Evergrande kwa mabao 2-1.

    Mchezo mwingine leo hii utakuwa ni wa nusu fainali ya kwanza utakaochezwa majira ya saa 7:30 mchana ambapo wenyeji Sanfrecce Hiroshima watavaana na River Plate.


     

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOMBE LA DUNIA LA VILABU:SAMATTA NA TP MAZEMBE YAKE DIMBANI TENA LEO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top