Basel,Uswisi.
Taarifa kutoka gazeti la michezo la Uswisi la Aargauer Zeitung na kunukuliwa na Metro ni kwamba Arsenal iko katika nafasi nzuri ya kumnasa kiungo Mmisri Mohamed Elneny baada ya klabu yake ya FC Basel kuripotiwa kukubali dau la paundi milioni 10m toka kwa miamba hiyo ya ligi kuu nchini England.
Tangu kuumia kwa viungo wake Francis Coquelin na Santi Cazorla Arsenal imekuwa ikihaha kutafuta kiungo wa kuilinda safu yake ya ulinzi inayoongozwa na Mfaransa Laurent Koscienly na Mjerumani Per Mertesacker na ripoti zilizotoka leo na kunaswa na Soka Extra ni kuwa Elneny ambaye kwasasa yuko nyumbani kwao Misri kwa mapumziko baada ya ligi ya Uswisi kusimama kupisha sikuu ya Krismasi na Mwaka Mpya anatarajiwa kusafiri kwenda Basel wiki ijayo kabla ya kutua London tayari kufanyiwa vipimo katika klabu ya Arsenal.
0 comments:
Post a Comment