Istanbul,Uturuki.
Chama cha soka cha Uturuki "Turkish Football Federation" (TFF) kimeamuriwa na mahakama ya jiji la Istanbul kumlipa fidia Halil Ibrahim Dincdag baada ya kumfutia leseni yake ya uwamuzi kwa kuwa ni shoga
Mahakama hiyo imeiamuru TFF kumlipa Halil Ibrahim Dincdag Laira za Kituruki 23,000 ($7,900).Aidha kiasi hicho ni kidogo kikilinganishwa na kile cha Laira 110,040 ($38,000) kilichotakiwa na wakili wa Dincdag katika kesi hiyo iliyofunguliwa ili kupinga dhuruma na unyanyasaji wanaofanyiwa mashoga na wasagaji nchini Uturuki.
Katika utetezi wake TFF imedai kuwa iliamua kumuondoa Dincdag katika orodha yake ya waamuzi baada ya jeshi la nchi hiyo alilokuwa pia akilifanyia kazi kumtimua baada ya kugundua kuwa ni shoga
Utetezi wa TFF umeendelea kudai kuwa maamuzi ya kumtema Dincdag pia yalilenga kulinda hadhi ya soka la nchi hiyo huku pia ikisisitiza kuwa mtu anayejihusisha na ushoga huwa hayuko sawa kimwili hivyo hawezi kuendaa na mikikimikiki ya uwanjani.
Dincdag alikuwa akifanya kazi za uwamuzi katika mkoa wa Trabzon kabla ya mwaka 2009 kufutiwa leseni yake kufuatia kujitangaza hadharani kuwa ni shoga.
0 comments:
Post a Comment