Timu ya JKT Ruvu leo imeondoka na Ushindi mnene baada ya kuichakaza Tanzania Prisons kutoka Mbeya jumla ya magoli 4 – 1.
Michael Aidan wa Ruvu, ndiye alianza kuziona nyavu za Prisons katika dakika ya 10 ya mchezo kabla ya kupachika goli lingine la pili katika dakika ya 31 ya mchezo huo.
Dakika 2 baadae, Mussa Juma alipachika goli la tatu ikiwa ni dakika 4 kabla ya Mohamed Mkopi wa Prisons kufunga bao pekee la kufutia machozi katika dakika 38 ya mchezo.
Samuel Kamuntu alizima kabisa nguvu ya Tanzania Prisons baada ya kufunga bao la nne na la mwisho katika mchezo huo mnamo dakika ya 70.
Katika mchezo mwingine, Coastal Union wametoka droo ya goli 1 – 1 dhidi ya African Sports katika mechi iliyopigwa katika uwanja wa Mkwakwani.Goli la Coastal lilifungwa na Juma Mahadhi huku lile la African Sports likifungwa na Mohamed Mtindi.
0 comments:
Post a Comment