MADRID,HISPANIA
Real Madrid imepata ushindi wa kihistoria baada ya jioni ya leo kuichabanga Rayo Vallecano kwa mabao 10-2 katika mchezo mkali wa ligi ya La Liga uliopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu.
Real Madrid ambayo wiki iliyopita ilikubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Villarreal leo ilionekana kuchangamka na kuonekana moto zaidi kwa Rayo Vallecano ikitumia washambuliaji wake mahiri wanaoitwaa BBC [Benzema,Bale na Ronaldo] ambao katika mchezo wa leo wamefunga jumla ya mabao 9.
Gareth Bale amefunga mabao 4,Benzema 3,Ronaldo 2 na Danilo 1
0 comments:
Post a Comment