Munich,Ujerumani.
BAYERN MUNICH kupitia kwa mtendaji wake mkuu Karl-Heinz Rummenigge imetangaza rasmi kuwa kocha wake mkuu Pep Guardiola ataachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na nafasi yake itazibwa na Muitaliano Carlo Ancelotti.
Guardiola (44) ambaye amekuwa akihusishwa na kutaka kutimkia England na kujiunga na vilabu vya Manchester United,Manchester City na Chelsea amegoma kuongeza mkataba wa kuendelea kuifundisha Bayern Munich hali iliyofanya uongozi utafute kochs mpya.
Guardiola alijiunga na Bayern Munich mwaka 2013 baada ya kuachana na FC Barcelona na tangu wakati huo amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya Bundesliga na moja la DFB Pokal
Ancelotti (56) aliyewahi kuvinoa vilabu vya AC Milan,Chelsea na Real Madrid anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na miamba hiyo ya Ujerumani.Mkata huo utakaoanza rasmi Julai 1,2016 unatarajiwa kufikia tamati June 30,2019.
0 comments:
Post a Comment