Tanga,Tanzania.
Goli la dakika ya 95 lililofungwa na kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko limeipa Yanga ushindi wa goli 1-0 dhidi ya African Sports katika mchezo pekee wa ligi kuu uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Mkwakwani,Yanga.
Goli hilo limepatakana baada ya mlinzi wa kushoto Hadji Mwinyi Mngwali kuambaa na mpira upande wa kushoto na kisha kupiga krosi nzuri iliyopanguliwa na kipa wa African Sports na kumkuta Donald Ngoma aliyetoa pasi ya kichwani kwa Thabani Kamusoko aliyefunga kwa shuti kali.
Kufuatia ushindi huo Yanga imekwea kileleni mwa ligi kuu baada ya kufikisha pointi 37 na kuishusha Azam FC yenye pointi 36 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
0 comments:
Post a Comment