728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 17, 2014

    MJUE MTUNZI WA WIMBO WA LIGI YA MABINGWA

    Habari na Paul Manjale

    Tony Britten:Huyu ndiye mtunzi wa wimbo maarufu wa ligi ya mabingwa Ulaya.Wimbo huo ambao uko katika lugha za Kiingereza,Kifaransa na Kijerumani ulitungwa mwaka 1992 wakati wa kuanzishwa kwa mfumo mpya wa michuano hii ambao tuko nao mpaka sasa.Britten hakutunga wimbo huo kwa ajili ya kujifurahisha yeye bali ilikuwa ni matakwa ya chama cha soka barani Ulaya kuwa na wimbo wake ambao utatambulisha michuano hiyo.Wimbo huo umeimbwa na waimbaji wa Academy of St.Martin iliyoko Uingereza.


    JE,JOAO BAPTISTA MARTINS NI NANI?
    Huyu ndiye mfungaji wa goli la kwanza la michuano hii mwaka 1955 ilipoanza rasmi ilikuwa ni katika mchezo wa hatua ya makundi kati ya Sporting Lisbon na Partizan Belgrade katika mchezo ulioisha kwa vilabu hivyo kutoka sare ya goli 3-3.Baptista alikuwa akiichezea Sporting wakati huo,huku ubingwa wa kwanza ukitwaliwa na klabu ya Real Madrid baada ya kuibamiza klabu ya Reims kwa goli 4-3.Shukrani kwa magoli ya Alfredo Di Stefano,Narquiton na Hector Rial aliyefunga mara mbili.Baptista alifunga goli hilo dakika ya 14 ya mchezo huo ulipigwa Sept 4 jijini Lisbon katika dimba la Nacional.
     Francisco "Paco" Gento López

    Ni mshindi mara sita wa taji hili aliwa na klabu ya Real Madrid miaka 1956, 1957, 1958, 1959, 1960 na 1966.


    KIKOMBE
    Kombe la ligi ya mabingwa  lina urefu wa sentimeta 74 na limetengenezwa kwa shaba mwaka 1967,lina uzito wa kilo 11.Lilitengenezwa na Jorg Stadelmann sonara toka Bern,Uswisi kwa gharama ya pesa za Kiswisi 10,000 (Swiss Francs).Hili ni kombe la pili baada ya lile la awali kutwaliwa moja kwa moja na klabu ya Real Madrid mwaka 1966 kama heshima ya kulinyakua mara ya sita.




    Timu yoyote ambayo hutwaa taji hilo mara tatu mfululizo ama mara tano kwa ujumla wake hupewa heshima ya kulitwaa kombe hilo moja kwa moja.Timu ambazo zimepata heshima hiyo ni Real Madrid,Ajax,Bayern Munich,Ac Milan na Liverpool.


    Pamoja na kikombe pia hutolewa jumla ya medali 40 za dhahabu kwa mshindi huku mshindi wa pili nae huvuna jumla ya medali 40 za fedha.(Hii ni kuanzia mwaka 2012 mpaka sasa).
    Kikosi cha Real Madrid ambacho kilitwaa ubingwa wa kwanza wa Ulaya
    JE,MALIPO YAKOJE?

    Kama waswahili wasemavyo kazi na dawa basi ndivyo ilivyo hata katika michuano hii  ambapo kila hatua timu shiriki kujikusanyia kitita fulani cha pesa.Mchanganuo uko kama ifuatavyo nah ii ni katika Euros.
    ·         Mtoano:2,100,000
    ·         Makundi: 8,600,000
    ·         Ushindi(Kila mchezo hatua ya makundi): 1,000,000
    ·         Sare(Mchezo wa makundi): 500,000
    ·         Hatua ya 16 bora: 3,500,000
    ·         Robo fainali: 3,900,000
    ·         Nusu fainali: 4,900,000
    ·         Mshindi wa pili: 6,500,000
    ·         Bingwa: 10,500,000

       WADHAMINI: 
       

     
    Michuano hii ina jumla ya wadhamini wanane wakuu ambao ni Master Card,Sony,Playstation,Nissan,Gazprom,Heineken,UniCredit na HTC pamoja na Adidas na Konami’s Pro Evolution Soccer kama wadhamini wadogo daraja la pili.


    JE,ADIDAS NI NANI KATIKA MICHUANO HII?
    Adidas mbali ya kuwa ni moja kati ya wadhamini wakubwa wa michuano hii pia ndiyo  kampuni pekee yenye haki ya kutengeneza mipira  na jezi za waamuzi wote wanaochezesha michuano hii.
     

    JE,HEINEKEN NI NANI?

    Heineken hawa  ni wadhamini wakubwa zaidi kuliko AdidasKampuni hii ya kutengeneza pombe ndiyo iliyochukua nafasi kubwa zaidi katika michuano hii.Ila kama ilivyokawaida katika jambo lolote lile changamoto huwa hazikosi sasa sikia hii.

    Heineken ni marufuku katika nchi za Ufaransa,Kazakhstan,Urusi,Uturuki na Slovenia,udhamini wa pombe michezoni hauruhusiwi katika nchi hizo.Hivyo katika nchi za Ufaransa,Uswisi na baadhi ya maeneo ya Hispania nafasi ya Heineken huchukuliwa na “Enjoy Responsibly” ama “Open your world”.Katika nchi za Urusi,Uturuki na Kazakhstan,udhamini huwa mikononi mwa Respect.

    VIPI UMRI WA WAAMUZI?
    Tangu mwaka 1990 waamuzi wa michuano hii hawapaswi kuwa na umri unaozidi miaka 45.Mwamuzi akifikisha umri huo huachia ngazi hata kama alikuwa bora kiasi gani.Kigezo hicho kimewekwa ili kuhakikisha waamuzi wote wanakuwa vizuri kiafya.
    Collina mmoja kati ya waamuzi bora zaidi wa michuano hii
    TUNAKARIBISHA MAONI KWA AJILI YA KUBORESHA BLOG HII JISIKIE HURU KUONGEA CHOCHOTE KILE CHENYE KUJENGA.......ASANTENI!!



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MJUE MTUNZI WA WIMBO WA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top