Aliyekuwa mkurugenzi wa klabu wa klabu ya Real Madrid na
mshindi wa kombe la dunia la mwaka 1986 na timu ya taifa ya Argentina Jorge
Valdano amesema kocha Jose Mourinho hayuko daraja moja na kocha wa Bayern
Munich Muhispania Pep Guardiola.
Valdano aliyeichezea Real Madrid miaka ya themanini na
kubahatika kuifundisha miamba hiyo kwa miaka miwili alifukuzwa katika nafasi
yake ya ukurugenzi mwaka 2011baada ya kushindwa kuelewana na Jose Mourinho
ambaye wakati huo alikuwa akiifundisha klabu hiyo.
Akiongea katika uzinduzi wa kitabu chake kiitwacho “The 11 Powers of a League” Valdano alisema
“Kama Guardiola ni Mozart,Mourinho ni Antonio Salieri (Mtunzi mahiri wa muziki
toka Italia) ambaye angeweza kuwa mwanamuziki mkubwa kama Mozart asingekuwepo
duniani”
Valdona aliongeza “Wakati
Guardiola akitwaa vikombe viwili vya ligi ya mabingwa ndani ya miaka mitatu na
klabu ya Barcelona,Mourinho alishindwa kuifikisha Real Madrid japo nusu fainali
katika kipindi chote alichokuwa hapo kama kocha licha ya kuwa na moja kati ya kikosi
bora zaidi katika historia ya klabu
hiyo.Mara zote alikuwa akitolewa mapema katika michuano hiyo.Hiyo ni changamoto
kubwa aliyoshindwa kuishinda”.
0 comments:
Post a Comment