ALLEN
KAIJAGE aka Middle ya juu
0655106767
Mambo
mengi na ya ajabu yanaendelea kutokea Duniani.Kati ya mambo yote hayo hakuna jambo jipya.Kinachofanyika kwenye
dunia ya sasa ni muendelezo ya yaliyofanyika awali.teknolojia mpya zinafanya
mambo yaonekane mapya wakati yameshafanyika.Asikudanganye mtu kuwa yeye ni
mgunduzi,Wagunduzi wote walishagundua zamani na kutuachia ugunduzi wao kwenye
makaratasi.Wakina newton na faraday ndio wagunduzi ila kizazi cha leo ni
wabunifu kutoka kwenye kile walichokigundua wakina newton.
Kwenye
ubunifu ndipo kuna vita ya fikira.Ndipo kwenye msuguano wa akili na ushindani
wa maarifa.Ili uwe mbunifu lazima uwe na maarifa kutokana na kusoma,kusikia au
kuona.unaweza ukasoma,ukasikia na kuona ila usielewe nini umesoma,kusikia au
kuona.Hapa ndipo inabidi ushirikishe ubongo wako kutafakari kile ulichosoma
kuona au kusikia.
Kufikiri
ndiko kunaleta matabaka,Ukiona mtu amekuzidi maendeleo ujue amekuzidi
kufikiri.Mnaweza kuwa na akili sawa mkasoma kitabu au shule moja baada ya
kumaliza kusoma mwenzako akafanya mambo
makubwa na wewe ukawa na maendeleo ya mwendo wa jongoo au usiwe na maendeleo
kabisa hapo ujue kabisa mwenzako alisoma na kuelewa na kuanza kufikiri jinsi
atakovyobadilisha nadharia kuwa vitendo,ila wewe tutakuita masikini wa fikra
maana ulisoma ukamaliza bila kuelewa na kutafakari ulichosoma.
Watanzania tumekua na macho lakini hatuoni,tuna masikio lakini hatusikii
pia tunasoma ilihali atuelewi.Kila siku tumekuwa watu wa majonzi na soka
letu.Leo tukipiga hatua moja mbele kesho tutarudi hatua tatu nyuma.Kila siku
tumekuwa tukitafuta ni nani mchawi wa
soka letu huku tukisahau kuwa tumejiloga wenyewe kwa kupiga kufuli bongo
zetu.Viongozi wetu kabla ya kuingia madarakani huwa na mawazo mazuri sana ila
ghafla akili zao uingia doa pale tu wanapopewa dhamana ya kuongoza soka letu.
Kuna vitu
unaweza ukafanikisha kwa njia za mkato ila sio soka.Tff wanalazimisha shubili
kuwa asali.Wanamawazo na fikra nyepesi katika mambo mazito.Tangu uongozi mpya
umeingia madarakani wamekuwa wakibuni mambo mengi sana wakihisi kuwa mwarobaini
wa timu ya taifa na soka letu kwa ujumla,Lakini hakuna hata moja lililosaidia
kati ya hayo mengi.Wamekua wakipoteza muda mwingi kuwaza juu ya maono mapya ya
stars bila kupata jawabu wakati majawabu
wanayaona,ni swala la kupiga chabo nchi jirani na kuhamisha majibu kwenye
makabrasha yao kwa faida ya nchi.
Kuna vitu vingine vya kawaida sana kufanya,hauhitaji
kua na akili za newton ili kujua nini waliofanikiwa walifanya mpaka kufikia
mafanikio yao.Tff wana mifano mingi wa nchi jirani zilizofanikiwa kwenye soka.Kwanini
tff wanashindwa kujifunza kutoka kwenye mifano hiyo? Nchi kama Angola ni nchi
ndogo kulinganisha na Tanzania tena nchi masikini ukilinganisha na nchi
yetu,Lakini Angola wamefanikiwa kisoka kuliko Tanzania,Kwanini tusijifunze
kutoka kwa angola.Nchi ndogo na masikini zaidi ya sisi inafanikiwa kwanini sisi
tushindwe?.Angola wametangulia kufikiri kama hawajatuzidi kufikiri.Angola si
nchi ya kwanza kufanikiwa,hapo awali nao walikua na akili zilizoganda kama
zetu.Waliamua kufikiri tofauti na hatima yake wakafanikiwa mpaka kufuzu kombe
la dunia mwaka 2006.Labda tff hawajasikia walichofanya angola pia hawajasoma
wala kuona walichokifanya hawa jirani zetu.
Tff wamesahau kuwa hakuna jipya kwenye
soka.Tff hawajui kuwa timu zote zilizofanikiwa nazo zilijifunza kwa
waliowatangulia kufanikiwa.Tanzania tunao majirani waliofanikiwa lakini
tunaogopa kuwaoigia chabo ili nasisi tufaulu.Hawakumbuki hata timu
zilizofanikiwa nazo zilipiga chabo na zikafanikiwa.Hao Angola kwenye mafanikio
yao walikopi kila kitu kutoka kwa wareno.Nchi kama senegal na mali zilikopi
kila kitu kutoka kwa wafaransa,sijui Tff
yangu inasubiri nini? Dunia ya sasa hauhitaji kutumia akili nyingi ili
kufanikiwa.Haswa huu ulimwengu wetu wa dijitali kila kitu kinajieleza
chenyewe.Tumeshindwa kugundua, tutashindwaje hata kuhamisha majibu kwenye
karatasi ya jirani ilihali macho tunayo.
Tff
haina haja ya kwenda kujifunza Brazil au Ujerumani kabla ya kujifunza kwa majirani.Wanachohitaji
watanzania kwa sasa ni kupiga hatua moja mbele kama walivyofanya majirani zetu
mfano Angola, Ghana na Nigeria.Tff inabidi ikajifunze kutoka kwenye nchi hizo
kwanza na kujua ni njia gani nchi hizo wametumia kufika hapa walipo.Ikiwezekana
tff wakopi mfumo mzima wa uendeshaji soka wanaotumia nchi hizo na kuhamishia
nchini.Hakika tutafanikiwa kwenye ubunifu huu wa kukopi.Nafikiri hii ndio itakua njia rahisi kwetu kufikia
mafanikio yetu.
0 comments:
Post a Comment