Habari na Paul Manjale
Klabu ya Simaba imewapa zawadi ya wikendi mashabiki wake
baada ya jioni ya leo kuibamiza klabu ya Gor Mahia ya Kenya kwa jumla ya magoli
3-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa katika dimba la uwanja wa
taifa jijini Dar es salaam.
Klabu ya Simba ambayo mwezi uliopita ilipokea kichapo cha
mbwa mwizi toka kwa klabu ya Zesco ya Zambia iliuanza mchezo wa leo kwa umakini
mkubwa lakini haikuweza kupata bao lolote katika kipindi cha kwanza kutokana na
washambuliaji wake kushindwa kuzitumia nafasi walizozipata.
Kiongera akishangilia goli dhidi ya Gor Mahia (Picha na bin zubery) |
Baada yakuanza kwa kipindi cha pili klabu ya Simba ilionekana
kuchangamka zaidi na kulisakama lango la Gor Mahia kama nyuki na kufanikiwa
kupata magoli matatu huku mshambuliaji wake mpya toka Kenya Paul Kiongera akiifunga
magoli mawili klabu yake hiyo ya zamani huku Ramadhan Singano maarufu kama
Messi akifunga goli moja.
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete