728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 12, 2014

    UJIO WA WAGENI NA ANGUKO LA SOKA YETU

    MAKALA YA LEO
    Na Thomas Sauli

     
    Soka la bongo limetawaliwa na wageni kwa miaka ya hivi karibuni,  timu zetu kubwa hasa Simba na Yanga zimekua zikisajili wachezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani !! Je ujio wa wageni una faida katika kukuza soka letu? Kusajili wageni sio jambo baya hata kidogo kwa sababu wanaleta kitu kipya katika soka letu.

    Lakini je wageni waliopo wanaleta kitu? Jibu ni hapana,  kwa maswali hayo hapo juu ni kwamba kwanza wageni walio katika ligi yetu viwango vyao wakati mwingine ni vidogo hata kuwazidi wachezaji wetu. Tatizo ni kwamba watanzania tumekua hatuthamini vya kwetu hata kama vina ubora kiasi gani na badala yake tunavipa kipaumbele vitu vya nje hata kama ni vibovu.


      Wachezaji wageni katika soka la bongo wanapewa mikataba minono na kulipwa mishahara mikubwa pamoja na kupewa huduma zote muhimu  wakati viwango vyao ni sawa na wachezaj wetu ambao mikataba yao ni ya kuunga unga. Ujio wa wageni pia unachangia kutopewa nafasi kwa vijana katika timu zetu mfano Simba na Yanga wachezaj wote wa kigeni wana nafasi za kudumu  katika vikosi vyao hii imeleta ugumu kwa wachezaji  wazawa wanaochipukia kupata nafas za kucheza walau mechi moja mfano kina Issa Ngao, Salum Telela na wengine wengi.

     Sakata la Okwi kugombewa na timu za simba na yanga linaonesha udhaifu mkubwa kwamba viongoz wa timu hizo mbili wanaamini kwamba hakuna wachezaji wengine wenye kiwango zaidi ya Okwi ama sawa na Okwi?  Pia viongozi wa vilabu vyetu wamelitupa soka la vijana na badala yake wanajiingiza katika migogoro ya kugombea wachezaji kutoka nje kama ilivyo kwa okwi.

     TFF nayo imeingizwa kwenye mkumbo huo wa kuwakumbatia wachezaji wa kigeni. Pia ujio wa wageni umepelekea wachezaji wengi wazawa kutemwa na vilabu vyao ili kupisha wageni Mustakabali wa soka letu upo mikononi mwa vilabu vyetu kuachana na kina Jaja na kuendeleza soka la vijana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UJIO WA WAGENI NA ANGUKO LA SOKA YETU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top