Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Ac Milan maarufu kama
Rossoneri Mbrazil Alexander Pato ambaye kwa kwasasa anakipiga na klabu ya
nyumbani kwao ya Sao Paulo ameilaumu klabu hiyo ya jiji la Milan kuwa ndiyo
sababu ya kuharibu soka yake kutokana na majeruhi ya mara kwa mara aliyokuwa
akiyapata.
Pato akiwa na jezi ya Sao Paulo |
Pato ambaye allichezea Milan jumla ya michezo 117 na
kufanikiwa kufunga jumla ya magoli 51 kati ya mwaka 2007 na 2012 akifanya
mahojiano na kituo kimoja cha habari cha nchini Brazil amesema Ac Milan
haikujali afya yake na badala yake ilimuwahisha kurudi uwanjani hata kabla
hajapona vizuri.
Pato akiwa na jezi ya Ac Milan |
Anasema “Nilipoanza kupata
majeruhi nilisafiri karibu dunia nzima kwa ajili ya matibabu,lakini tatizo
lilikuwa ni muda wa matibabu/kupona,niliwahishwa kurejeshwa kiwanjani.Klabu
iliangalia maslahi yake tu huku ikiiacha afya yangu ikiteketea na hatimaye soka
yangu kushuka.
Pato akiwa na jezi ya Brazil |
“Hii imebainika baada ya vipimo nilivyofanyiwa
hapa Brazil na kugundulika kuwa tatizo halikuwa langu.Huu ni msimu wangu wa
pili hapa nikiwa na vilabu ya Corinthias na Sao Paulo sijapata majeruhi yoyote
kwasababu afya yangu inaangaliwa.Alimaliza Pato
0 comments:
Post a Comment