Mmiliki wa klabu ya Newcastle United inayoshiriki ligi kuu ya Epl Mike
Ashley anafikiria kuipiga bei klabu hiyo inayotumia dimba la St.James Park kwa
mechi zake za nyumbani ili aweze kuwa huru kuinunua klabu ya Rangers ya
Scotland.
Mike Ashley |
Ashley ambaye aliinunua Newcastle United mwaka 2007 kwa kitita cha paundi
milioni 134 anapanga kuipiga bei klabu hiyo kwa paundi milioni 230 amekuwa
katika mvutano wa mara kwa mara na mashabiki wa klabu hiyo hasa katika masuala
mazima ya uendeshaji wa klabu na usajili wa wachezaji.
Mmiliki huyo ambaye tayari ameshafanikiwa kujipenyeza na hatimaye
kumiliki hisa kadhaa za umiliki wa uwanja wa Ibrox unaotumiwa na klabu ya
Rangers kwa mechi zake za nyumbani anaona njia pekee ya kuachana na misuguano
ya mara kwa mara na mashabiki wa Newcastle ni kuiuza klabu hiyo na kuinunua
Rangers na hatimaye kuirejesha ligi ya mabingwa.
Wachezaji wa Newcastle wakipambana na Gervinho |
Rangers ambayo kwa miaka mitatu mfululizo imekuwa ikikabiliwa na hali
mbaya ya kiuchumi hata kufikia kushushwa daraja inaonekana kama ni jibu kwa
Mike Ashley ambaye kiu na ndoto yake kubwa imekuwa ni kumiliki timu
inayoshiriki ligi ya mabingwa.Kwakuwa shirikisho la vyama vya soka barani Ulaya
Uefa haliruhusu mmiliki mmoja kuwa na timu mbili katika michuano iliyo chini
yake Ashley hana budi zaidi ya kuachana na Newcastle United.
Wakati huohuo Mike Ashley amempa mechi mbili tu kocha wa timu hiyo
Alain Pardew ili kuokoa kibarua chache vinginevyo atamtimua mara moja.Pardew
ambaye mwaka 2012 alipewa mkataba mrefu wa miaka minane kuendelea kukinoa
kikosi hicho ameshindwa kushinda mchezo wowote kati ya mitatu ya ligi akiwa na
klabu hiyo ya St.James Park msimu huu.
Alan Pardew kocha wa Newcastle |
Kwa mujibu wa Ashley mechi zitakazomuokoa au kumuangamiza Pardew ni ile
ya jumamosi dhidi ya Southampton na ile itakayofuata dhidi ya Hull City.Mapema
wiki iliyopita Mike Ashley alianza kumshambulia kocha huyo kwa kumwambia kuwa
hakustahiri kupanga wachezaji watano wa kikosi cha kwanza katika mchezo wa
kombe la Capital One dhidi ya timu kibonde ya Gillingham.Pia mmiliki huyo
ambaye ametumia paundi milioni 35 katika usajili wa nyota tisa klabuni hapo
anaona kwamba Pardew hana kisingizio cha kuendelea kufanya vibaya na badala
yake ahakikishe anashinda michezo hiyo miwili muhimu.
0 comments:
Post a Comment