Habari na Paul Manjale
Kiungo wa klabu ya Manchester City Mfaransa Samir Nasri amesema
klabu ya Liverpool haitokuwa tena tishio msimu huu katika mbio za kuwania
ubingwa wa Epl kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo ilimaliza ikiwa nafasi ya
pili pointi mbili nyuma ya City waliotwaa ubingwa huo siku ya mwisho.
Nasri akiwa na taji la Epl |
Badala yake Nasri amevipa nafasi vilabu vya Chelsea na
Manchester United kutoa upinzani mkubwa kwa klabu yake msimu huu.Nasri anadhani
kuwemo kwa Liverpool katika michuano ya ligi ya mabingwa na kuondoka kwa
mshambuliaji wake mahiri Louis Suarez aliyetimkia klabu ya Barcelona
kutaidhorotesha klabu hiyo kwa kiasi kikubwa.
Nasri akiwajibika uwanjani |
Aliongeza “Chelsea
walikuwa na kikosi kizuri msimu uliopita lakini tatizo lao lilikuwa n katika
safu yake ya ushambuliaji ambayo kwa sasa imepata suluhisho baada ya kutua kwa mshambuliaji
Diego Costa.Manchester United bado naipa nafasi ya kufanya vizuri licha ya
kuanza vibaya michezo yake ya ligi.Kitakachoisaidia United ni usajili mkubwa na mzuri ilioufanya pamoja na kutokuwa na michuano mingi msimu
huu.Arsenal bado siwapi nafasi kwani bado wana mapungufu makubwa katika kikosi
chao. Alimaliza nyota huyo
Nasri akifanya mazoezi kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa |
0 comments:
Post a Comment