Wakati
kiungo wa klabu ya Manchester City Frank Lampard akifunga bao dhidi ya klabu
yake ya zamani ya Chelsea na kujizuia kushangilia na hatimaye kuufanya mtanange
wa ligi kuu ulivikutanisha vigogo hivyo siku ya jumapili uishe kwa sare ya bao
1-1 hali ilikuwa ni tofauti kidogo katika mji wa Bombo huko Uganda baada ya
shabiki mmoja kuripotiwa kufariki dunia.
Shabiki
huyo ambaye amefahamika kwa jina la Fahad Musana (24) ni mchezaji wa klabu ya
Simba inayoshiriki ligi kuu ya Uganda maarufu kama (UPL).Musana ambaye
inasemekana alikuwa ni shabiki wa kutupwa wa klabu ya Chelsea alikutwa na
umauti huo njiani akiwahishwa hospitali ya jeshi ya Bombo muda mfupi baada ya
kiungo Frank Lampard kuifungia klabu yake mpya ya Manchester City bao la
kusawazisha.
Marehemu Fahad Musana |
Taarifa
za kuaminika zinasema Musana ambaye aliiongoza klabu yake ya Simba kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Entebe Fc siku ya jumamosi katika uwanja
wa Nakivubo alikuwa akiufuatilia mtanange huo kupitia televisheni katika
ukumbi mmoja mashuhuri mjini hapo. Mashuhuda wa tukio hilo wanasema Musana alipoteza fahamu na kudodoka mara tu
Lampard alipofunga bao la kusawazisha.Musana
alifariki dakika chache baadae wakati akiwahishwa hospitalini kupatiwa
matibabu.
“Alikuwa
ni shabiki mkubwa wa Chelsea na alikuwa
tayari kufanya chochote kwa ajili ya klabu hiyo,mbali ya kuwa ni mcheza kamari
mkubwa (betting).Tulifanya nae mazoezi asubuhi ya jumapili na hata kupata
chakula cha mchana pamoja.Alisema Gerald Bagoole mfungaji wa bao pekee la Simba
jumamosi dhidi ya Entebe Fc wakati akifanya mahojiano na kituo cha Kawowo
Sports.
Hili
ni tukio la pili na la aina yake katika soka kwani mwaka jana jijini
Kampala,Uganda shabiki mmoja alijikuta akipoteza nyumba yake kwenye kamari
baada ya klabu anayoishabikia ya Arsenal
kufungwa goli 1-0 na Manchester United katika mchezo wa ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment