Habari na Paul Manjale
Mshambuliaji
mpya wa klabu ya Manchester United Mcolombia Radamel Falcao Garcia Zarate “El
Tigre” ameishukuru klabu yake ya zamani ya Monaco kwa kukubali kumwachia atue katika
klabu ya Manchester United kwa uhamisho
wa mkopo wa msimu mmoja wenye kipengele cha kuwa wa kudumu hapo baadae.
Akiongea
na mtandao wa Telefoot Falcao amesema “Nataka kuwashukuru watu wa Ufaransa kwa
kuniunga mkono kwa kipindi chote nilichokuwa hapa”.
“Binti
yangu alizaliwa hapa hivyo Monaco na Ufaransa kwa pamoja zitabaki kuwa moyoni
mwangu”
“Nataka
kuwashukuru watu wa Monaco kwa kunisaidia katika kipindi chote pamoja na kunipa
nafasi ya kutua Manchester United”
Wakati
huohuo klabu ya Manchester United imetupilia mbali uvumi ulioenezwa juu ya umri
halisi wa nyota wake huyo mpya raia wa Colombia na kusema wanaamini kuwa mchezaji huyo ana umri wa miaka
28 na siyo 30 kama ilivyovumishwa na vyombo mbalimbali vya habari hapo nyuma.
United
kupitia msemaji wake mkuu imesema haishitushwi na uvumi huo badala yake
inaamini kile kilichoandikwa katika hati ya kusafiria ya nyota huyo ambayo
inaonyesha kuwa Falcao alizaliwa tarehe 10 february mwaka 1986 na siyo
vinginevyo.
Hivi
karibuni kuliibuka uvumi kuwa Falcao alipunguza miaka miwili toka katika umri
wake halisi ili apate nafasi ya kucheza katika fainali za kombe la dunia la
vijana chini ya miaka 20 mwaka2005.Mwaka 2012 shule moja aliyosoma Falcao ilivujisha
taarifa zikisema kuwa nyota huyo alizaliwa mwaka 1984 hatua iliyopelekea
familia yake kuonyesha kwenye vyombo vya habari vyeti vya kuzaliwa vya nyota
huyo mwenye jicho la goli.
0 comments:
Post a Comment