Watford, England.
BAO la kiti taka la dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza la kiungo, Emre Can limeipa Liverpool pointi tatu muhimu baada ya kuiwezesha miamba hiyo ya Anfield kuifunga Watford kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu England uliochezwa usiku huu huko Vicarage Road.
Can amefunga bao hilo ambalo huenda likaingia kwenye kinyang'anyiro cha kusaka bao bora la msimu baada ya kuunganisha pasi safi ya Lucas Leiva akiwa katikati ya mabeki wawili wa Watford na kuutia mpira wavuni.
Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa Liverpool ikilazimika kufanya mabadiliko bila kupenda katika dakika 15 za kipindi cha kwanza baada ya kiungo wake Philippe Coutinho kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Lallana.
Ushindi huo umeifanya Liverpool ibaki nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 66.Pointi tatu mbele ya Man City na pointi nne mbele ya Manchester United inayoshika nafasi ya tano.
Vikosi
Watford (5-3-2): Gomes; Amrabat (Okaka,85),Mariappa, Prodl, Britos (Kabasele,19), Janmaat; Capoue (Success, 73),Doucoure, Cleverley; Niang, Deeney
Liverpool (4-3-3): Mignolet; Clyne, Matip,Lovren, Milner; Wijnaldum, Lucas, Can (Sturridge, 85); Firmino, Origi, Coutinho (Lallana, 13) (Klavan, 86)
0 comments:
Post a Comment