Dar Es Salaam,Tanzania.
NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude ameruhusiwa kutoka katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa amelazwa tangu jana kufuatia ajali ya gari iliyotokea eneo la Dumila mkoani Morogoro.
Akizungumza leo baada ya kutoka hospitalini hapo, Mkude amesema kwamba yuko vizuri na hana tatizo lolote ukiondoa michubuko kidogo.
“Daktari amesema ni mshituko tu baada ya ajali, lakini sijaumia popote na ninaweza kuendelea na ratiba zangu kama kawaida,”amesema
0 comments:
Post a Comment