Libreville,Gabon.
TIMU ya taifa ya Ghana ya vijana wa chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Black Starlets iliyoko nchini Gabon kwenye michuano ya AFCON imekumbwa na balaa baada ya wachezaji wake wachezaji watano wa kutumainiwa pamoja na kocha wao Mkuu,Paa Kwesi Fabin wote kwa pamoja kuugua ugonjwa wa malaria.
Taarifa kutoka mtandao wa michezo wa Ghana wa GHANASoccernet umesema balaa hilo limetokea usiku wa kuamkia jana Jumatatu hali iliyopelekea kuharibika kwa baadhi ya programu za mazoezi zilizokuwa zimepangwa kufanyika asubuhi.
GHANASoccernet imewataja wachezaji waliokumbwa na balaa hilo kuwa ni Edmund Ako-Mensah,Gideon Acquah,Abdul Razak Yusif,Isaac Antah pamoja na Faisal Osman.
Ghana inatarajiwa kushuka dimbani kesho Jumatano kucheza na Niger kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali utakaochezwa huko Port- Gentil.
Ghana ilitinga nusu fainali baada ya kuongoza kundi A kufuatia kupata ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Cameroon na mabao 5-1 dhidi ya wenyeji Gabon kabla ya kutoka sare ya bila kufungana na Guinea.
0 comments:
Post a Comment