728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 24, 2017

    Usajili:Newcastle United yachomoa mmoja kutoka kwa mabingwa Chelsea


    Sunderland,England.

    KLABU ya Newcastle United ambayo imerejea ligi kuu England msimu huu baada ya kushuka daraja msimu mmoja uliopita leo imemsajili moja kwa moja winga wa kimataifa wa Ghana,Christian Atsu kutoka klabu ya Chelsea kwa ada ya Pauni Milioni 6.

    Atsu mwenye miaka 25 amesaini mkataba wa miaka minne wa kuwatumikia mabingwa hao wa ligi daraja la kwanza baada ya kocha Rafa Benítez kuridhishwa na kiwango alichokionyesha msimu huu wakati akiichezea klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mmoja.


    Akiwa kwa mkopo Newcastle United,Atsu alifanikiwa kufunga mabao matano katika michezo 32 aliyoichezea klabu hiyo ya Saint James's Park.Akianza kikosi cha kwanza mara 15 huku mara 17 akitokea benchi.

    Atsu alijiunga na Chelsea mwaka 2013 akitokea FC Porto ya nchini Ureno kwa ada ya Pauni Milioni 3.5 lakini hakufanikiwa kucheza mchezo hata mmoja akiwa na kikosi cha kwanza na badala yake alijikuta akitolewa kwa mkopo kwenye vilabu vya Vitesse Arnhem,Everton, Bournemouth na Malaga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Usajili:Newcastle United yachomoa mmoja kutoka kwa mabingwa Chelsea Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top