728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 24, 2017

    Kisa Pua Sane kuikosa michuano ya kombe la mabara.


    Berlin,Ujerumani.

    WINGA wa Manchester City, Leroy Sane amejiondoa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kitakachoshiriki michuano ya kombe la mabara mwaka huu huko Urusi ili afanyiwe upasuaji wa pua yake.

    Sane mwenye umri wa miaka 21 ataikosa michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kuanzia Juni 17 huko nchini Urusi na kufikia tamati Julai 2.

    Pia ataukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Denmark utakaochezwa Juni 6 pamoja na mchezo wa kufuzu kombe la dunia utakaochezwa siku nne baadae dhidi ya San Marino. 

    "Ningependa kwenda Urusi lakini baada ya kufanya mazungumzo na timu ya madaktari,nimeamua kuyatumia majira haya ya joto kufanya upasuaji huo ili msimu ujao unikute nikiwa na afya nje kabisa.Amesema Sane.

    Kujitoa kwa Sane ni pigo kwa Kocha timu ya taifa ya Ujerumani,Joachim Low ambaye aliamua kutumia wachezaji vijana zaidi kwenye michezo ya mwaka huu na kuwaweka kando wazoefu.

    Sane alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji watatu wanaocheza ligi kuu England waliopata kutajwa kwenye kikosi cha Low.Wengine ni kiungo wa Liverpool,Emre Can na beki wa Arsenal,Shkodran Mustafi.

    Low ana mpaka Juni 7 mwaka huu kuwasilisha FIFA kikosi kamili tayari kwa michuano ya kombe la mabara.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kisa Pua Sane kuikosa michuano ya kombe la mabara. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top