Faridi Miraji , Dar es salaam.
Tanzania -Fainali ASFC
Simba Sc 2-1 Mbao Fc
Simba wamekuwa mabingwa wa kombe la shirikisho la Tanzania maarufu kama ASFC na kuwa wawakilishi wa Tanzania kwenye kombe la shirikisho Afrika baada ya miaka minne pia SIMBA wamewafikia wapinzani wao Yanga kwa kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho Mara nne Mara ya mwisho Simba kutwaa kombe hili ilikuwa mwaka 2000
England -Fainali FA cup
Arsenal 2-1 Chelsea
Mtu na bahati yake bhana Unajua Wenger mjanja Sana mechi ambazo unahic atafukuzwa ndio anafanya vzr Arsenal ameweka Historia ya kutwaa ubingwa wa FA cup Mara nyingi zaidi wametwaa Mara 13 moja zaidi ya Man United Mara 12.
Hispania -Fainal Copa Del Rey
Fc Barcelona 3-1 Deportivo Alvés
Baada ya kukosa makombe ya laliga, uefa sasa Barcelona wametoka na kitu kombe la 29 Copa Del Rey.
Germany -Fainali DFB Pokal
Frankfurt 1-2 Borrusia Dontmund
Baada ya kukosa Bundersliga Borrusia Dontmund wamefanikiwa kubeba kombe la DFB Pokal kombe la ujerumani
Fainali Coupe De France
Angers 0-1 PSG
Hawa nao wameweka Historia katika kombe la coupe de France kombe la Ufaransa Kwa kubeba Mara nyingi zaidi wamebeba mara 11. Baada ya kukosa Ligue 1 kwenda na Monaco, Borrusia Dontmund nao wanajipoza Kwa kombe la Ufaransa.
Scotland -Scottich Cup
Celtic 2-1 Aberdeen
Celtic wamebeba kombe la Mfalme la Scotland maarufu kama Scottich Cup
0 comments:
Post a Comment