Nairobi,Kenya.
BEKI wa kushoto wa Tusker FC ya Kenya,Shafik Batambuze amefichua kwamba amekataa kujiunga na AFC Leopards baada ya mabingwa hao mara 13 wa Kenya kushindwa kufikia dau alilopewa na Singida United ambayo imepanda daraja la ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Batambuze ambaye pia ni beki wa kutumainiwa wa timu ya taifa ya Uganda ametoa kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na kituo cha matangazo cha Capital Sports.
"Mimi ni msafiri na kwangu kilicho muhimu kuliko vyote ni ofa ambayo timu inakuwa imetoa.
Acha niwe mkweli,AFC Leopards walinifuata wakitaka kunisajili lakini nilipoiona ofa ya Singida United ilikuwa ni rahisi kwangu kufanya maamuzi.Nimekuwa hapa Kenya kwa kipindi kirefu.Najua hali za kiuchumi za vilabu vya hapa.Zisingeweza kufikia ofa ya Singida United.
Batambuze anatarajiwa kuichezea Tusker FC mchezo wake wa mwisho Jumapili hii pale watakaposhuka kwenye Uwanja wa Kinoru kucheza na Ingwe huko Meru.
Beki huyo anayejua vyema kuutumia mguu wake wa kushoto alijiunga na Tusker FC akitokea Western Stima aliyojiunga nayo akitokea Sofapaka kabla ya hapo alikuwa akiichezea Simba ya nyumbani kwao Uganda.
0 comments:
Post a Comment