728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 21, 2017

    Monaco yafunga msimu kibabe zaidi Ufaransa,PSG yabanwa


    Monaco,Ufaransa.

    MABINGWA wapya wa Ligue 1,AS Monaco wamefunga msimu wa ligi hiyo kibabe zaidi baada ya Jumamosi usiku kupata ushindi wake wa 12 mfululizo kufuatia ushindi wao wa mabao 3-2 walioupata ugenini Stade de la Route de Lorient dhidi ya wenyeji wao Rennes.

    Shukrani kwa mabao ya dakika za 42,47 na 78 ya Wabrazil Fabinho,Jemerson,na Jorge.Mabao ya Rennes yamefungwa na Adama Diakhaby dakika za 69 na 90.

    Ushindi huo ambao ni wa 30 kwa AS Monaco kuupata Ligue 1 msimu huu umeifanya miamba hiyo ya Stade Louis II imalize msimu ikiwa imeweka rekodi ya kufunga mabao 107 na kufikisha pointi 95 katika michezo 38 ya ligi hiyo ya kwanza kwa ukubwa nchini Ufaransa.Pointi 8 zaidi ya mabingwa wa zamani Paris Saint Germain walioshika nafasi ya pili.



    Msimu huu AS Monaco imetoka sare mara tano katika michezo 38 ikifunga jumla ya mabao 158 katika michuano yote na kuwa moja katika ya timu chache zenye safu bora zaidi ya ushambuliaji barani Ulaya.

    Katika mchezo mwingine uliochezwa Jumamosi usiku Paris Saint Germain ikiwa nyumbani Parc des Princess imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Caen.

    Marseille imeipiku Bordeaux na kumaliza katika nafasi ya tano na kufanikiwa kukata tiketi ya kucheza michuano ya Europa Ligi baada ya kuifumua Bastia kwa bao 1-0 lililofungwa na nahodha wake Batefimbi Gomis aliyekuwa anafunga bao lake la 20.

    Bastia na Nancy zimeshuka daraja huku Lorient iliyoshika nafasi ya 18 Ligue 1 ikilazimika kucheza na timu iliyoshika nafasi ya tatu Ligue 2 ili kujihakikishia kubaki ama kushuka daraja.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Monaco yafunga msimu kibabe zaidi Ufaransa,PSG yabanwa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top