Monaco,Ufaransa.
MABINGWA wa Ufaransa,AS Monaco wametangaza kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji,Youri Tielemans kutoka Anderlecht kwa ada ya uhamisho ya Euro Millioni 25.
Tielemans mwenye umri wa miaka 20 amesaini mkataba wa miaka minne utakaofikia tamati Juni 30,2022.
Tielemans anaiacha Anderlecht akiwa ameichezea jumla ya michezo 173.Msimu huu aliifungia timu hiyo mabao 13 katika michezo 37 na kuiwezesha miamba hiyo ya jiji la Brussels kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Ubelgiji.
0 comments:
Post a Comment