London,England.
WAGENI kwenye ligi kuu ya soka ya England,Brighton & Hove Albion wameanza mapema mikakati ya kukiimarisha kikosi chao tayari kwa msimu mpya baada ya kumsajili kiungo wa Ingolstadt ya Ujerumani, Pascal Gross.
Gross mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa miaka minne wa kuichezea Brighton & Hove Albion kwa ada ambayo haijawekwa wazi.
Msimu huu Gross amecheza michezo 32 kwenye ligi ya Bundesliga na kufunga mabao manne.Akifanikiwa kutengeneza nafasi 195 za mabao idadi ambayo ni kubwa kuliko wachezaji wote Bundesliga.
Gross alianzia soka lake kwenye klabu ya Hoffenheim aliyojiunga nayo mwaka 2008 kabla ya mwaka 2011 kujiunga na Karlsruhe.Mwaka 2012 alitua Ingolstadt ambayo mpaka sasa amefanikiwa kuichezea jumla ya michezo 154.
0 comments:
Post a Comment