Manchester,England.
KIUNGO Michael Carrick ataendelea kuvaa jezi ya Manchester United hii ni baada ya Jumamosi Usiku kusaini kandarasi mpya ya mwaka mmoja ya kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka Juni 2018.
Carrick mwenye umri wa miaka 35 sasa alijiunga na Manchester United miaka 11 iliyopita akitokea Tottenham kwa ada ya uhamisho ya £17m.
Katika kipindi cha miaka 11 alichohudumu katika klabu hiyo ya Old Trafford,Carrick amefanikiwa kuichezea Manchester United jumla ya michezo 459 akifunga mabao 24.
Pia ameshinda ubingwa wa ligi kuu mara tano.Ameshinda makombe mawili ya kombe la ligi (EFL).kombe moja la FA,Ngao ya jamii (Community
Shields) mara sita.Klabu bingwa Ulaya mara moja.Ubingwa wa kombe la dunia la vilabu na kombe moja la Europa ligi.
0 comments:
Post a Comment