728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 31, 2017

    Zambia yaigonga 4-3 Ujerumani na kufuzu robo fainali kombe la dunia la U20

    Jeju,Korea Kusini.

    TIMU ya taifa ya Zambia ya chini ya miaka 20,maarufu kama Young Chipolopolo imekuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu robo fainali ya michuano ya kombe la dunia la vijana wa umri huo baada ya jioni hii kutoka nyuma na kuwafunga vijana wenzao wa Ujerumani mabao 4-3 katika mchezo mkali wa hatua ya 16 bora uliochezwa huko Jeju,Korea Kusini kwa dakika 120.

    Mpaka dakika tisini (90) zinakamilika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 3-3.Ujerumani ndiyo waliokuwa kwa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Philipp Ochs aliyefunga kwa mkwaju wa faulo.



    Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Zambia ambayo ilikuja juu na kupata mabao matatu kwa Emmanuel Banda Enock Mwepu na Fashion Sakala.Mchezo ukiwa unaelekea mwishoni Ujerumani ilijipatia mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa Suat Serdar na Jonas Arweiler na kufanya mchezo uongezwe dakika 30 ili kumpata mshindi.

    Kipindi cha pili cha dakika za nyongeza kilishuhudia Shemmy Mayembe akifunga bao la nne kwa shuti Kali la karibu na kufanya mchezo umalizike kwa Zambia kushinda kwa mabao 4-3.

    Hii ni mara ya pili mfululizo Ujerumani inatupwa nje ya michuano na timu kutoka Afrika.Mara ya kwanza ilikuwa ni miaka miwili iliyopita Mali katika michuano iliyofanyika nchini New Zealand.


    Sasa Zambia itacheza robo fainali na mshindi kati ya Ufaransa ama Italia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Zambia yaigonga 4-3 Ujerumani na kufuzu robo fainali kombe la dunia la U20 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top