728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 23, 2017

    Baada ya Simba,Yanga SportsPesa yamwaga noti Singida United

                                       

    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya SportsPesa leo imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kuidhamini klabu ya Singida United ambayo imepanda daraja la ligi kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya kushuka daraja miaka 16 iliyopita.


                                        


    Kupitia mkataba huo uliosainiwa asubuhi ya leo Jijini Dar Es Salaam,Singida United itapata malipo ya Shilingi Milioni 250 kama malipo ya kuvaa jezi zenye nembo ya kampuni ya SportsPesa.

    Pia Singida United itapata bonasi ya Mamilioni mengine ikiwa itafanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara msimu huu.


                                             

    Nahodha wa Singida United,Nizar Khalfani akitambulisha jezi yenye nembo ya Sports Pesa.


    Singida United inakuwa timu ya tatu ya ligi kuu bara kuingia mkataba wa udhamini na SportsPesa baada ya vilabu vya Simba na Yanga kuingia mikataba ya miaka mitano mitano yenye thamani ya Shilingi Bilioni 5.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Baada ya Simba,Yanga SportsPesa yamwaga noti Singida United Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top