728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 22, 2017

    Kwa kauli hii ya Wenger, mashabiki Arsenal wala msitegemee usajili mkubwa


    London,England.

    LIGI kuu ya soka ya England imetia nanga hapo jana Jumapili jioni kwa mabingwa Chelsea kukabidhiwa mwali wao huku ikishuhudiwa vilabu vya Tottenham,Manchester City na Liverpool vikifanikiwa kumaliza katika nafasi nne za juu na kuiacha Arsenal kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20 ikishindwa kukata tiketi ya kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao na badala yake itacheza michuano ya Europa Ligi.

    Tayari kocha wa Arsenal Mfaransa,Arsenal Wenger ameshaanza kutoa kauli ambazo zinaweza zikazidi kuwatia simanzi zaidi mashabiki wa klabu hiyo ya Emirates ambao walidhani baada ya klabu hiyo kufanya vibaya msimu huu kocha huyo atafanya usajili mkubwa na wa maana baada ya kumaliza nje ya nafasi nne za juu.

    Wenger,67,ambaye hivi karibuni atatoa tamko la kama ataongeza mkataba klabu hapo ama ataondoka zake amesema Arsenal haihitaji kusajili usajili mkubwa kama wengi wanavyofikiria bali inahitaji kuongeza mchezaji moja tu au wawili wenye ubora kikosini ili iweze kuwa mshindani wa kweli ligi kuu England na ikiwezekana itwae kabisa ubingwa.

    Akifanya mahojiano na mtandao wa klabu hiyo,Wenger amesema kikundi cha wachezaji alichonacho kwa sasa kinatosha na kinaweza kufanya mambo makubwa hapo baadae iwapo kitaendelea kuwa pamoja.

    Amesema wachezaji wamejifunza mengi mpaka sasa hii ni baada ya kupitia nyakati nyingi ngumu sana msimu huu.

    Ameongeza kitu cha kwanza ambacho Arsenal inatakiwa kufanya kwa sasa ni kuhakikisha kuwa asilimia 90 ya wachezaji wake wanaendelea kubaki kikosini hapo kisha ataongeza mchezaji mmoja au wawili wa kukiimarisha kikosi na kusisitiza kuwa haitaji kundi kubwa zaidi la wachezaji wapya.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kwa kauli hii ya Wenger, mashabiki Arsenal wala msitegemee usajili mkubwa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top