Morogoro,Tanzania.
Kiungo wa Simba,Jonas Mkude amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Mitibora,Dumila mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam kuiwahi Taifa Stars.
Taarifa za awali zinasema Mkide ameumia maeneo ya shingoni, amekimbizwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro pamoja na majeruhi wenzie ambao baadhi wana hali mbaya.
Wakati huohuo taarifa zaidi zinasema shabiki mmoja kike aliyekuwa ndani ya gari hiyo amefariki dunia baada ya kupata majeraha makubwa mwilini.
0 comments:
Post a Comment