Libreville,Gabon.
TIMU ya vijana ya Mali sasa itacheza fainali ya AFCON U-17 na vijana wenzao wa Ghana hii ni baada ya usiku wa kuamkia leo kuwafunga vijana wenzao wa Guinea kwa penati 2-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali uliochezwa huko Stade de l’Amitie, Libreville,Gabon.
Mchezo huo ulilazimika kumpata mshindi kwa kutumia changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kushindwa kufungana katika dakika 90 za kawaida licha ya kushambuliana kwa zamu.
Shujaa kwa upande wa Mali ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hilo alikuwa ni mlinda mlango wake,Youssouf Koita aliyedaka penati tatu za Guinea huku moja ikipaa juu ya lango.
Penati za Mali zimefungwa na Hadji Drame pamoja na Fode Konate.Mchezo wa fainali utachezwa Jumapili Mei 28 huko Libreville.
0 comments:
Post a Comment