728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 22, 2017

    Ratiba Nusu Fainali AFCON U17


    Port Gentil,Gabon.

    HATUA ya makundi ya michuano ya Afrika kwa vijana (AFCON U17) imehitimishwa jana Jumapili usiku kwa michezo miwili ya kundi B kuchezwa katika miji ya Libreville na Port Gentil na kushuhudia timu za Mali na Niger zikifuzu nusu fainali baada ya kupata ushindi dhidi ya Angola na Tanzania.

    Katika mchezo wa kwanza uliochezwa huko Libreville, Mali iliifunga Angola mabao 6-1 na kumaliza ikiwa kileleni mwa msimamo wa kundi B baada ya kujikusanyia pointi saba.

    Katika mchezo wa pili uliochezwa huko Port Gentil ilishuhudiwa Niger ikifuzu kwa mara ya kwanza hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Tanzania kwa jumla ya bao 1-0 bao lililopatikana katika kipindi cha kwanza.




    Matokeo hayo mbali ya kuzipa Mali na Niger tiketi ya kufuzu nusu fainali ya AFCON pia yamezipa timu hizo tiketi ya kucheza michuano ya kombe la dunia la vijana litakalofanyika mwezi Octoba mwaka huu huko nchini India.

    Mali imefuzu kombe la dunia kwa mara ya tano sasa.Awali ikiwa ni mwaka 1997,1999, 2001 na 2015 huku Niger ikiwa ndiyo mara yao ya kwanza kufuzu.

    Michezo ya nusu fainali itachezwa Jumatano Mei 24 ambapo saa 11:30 jioni,Ghana itacheza na Niger huko Port Gentil wakati saa 2:30 jioni, mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mali watamenyana na Guinea huko Libreville.

    Mchezo wa fainali utachezwa Jumamosi Mei 28 mwaka huu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ratiba Nusu Fainali AFCON U17 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top