Stockholm,Sweden.
MANCHESTER United imetwaa ubingwa wake wa pili msimu huu na wa kwanza katika historia ya michuano ya Europa Ligi baada ya Jumatano usiku kuifunga Ajax mabao 2-0 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa huko Friends Arena jijini Stockholm,Sweden.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Damir Skomina kutoka nchini Slovenia,ilishuhudiwa Manchester United wakitumia uzoefu wao na kufanikiwa kukibana vyema kikosi cha Ajax kilichokuwa na kimesheheni vijana wengi.
Paul Pogba alianza kuiandikia Manchester United bao la kuongoza katika dakika ya 18 baada ya shuti lake kumbabatiza beki wa Ajax Davinson Sanchez na kutinga wavuni na kumwacha mlinda mlango Andres Onana akiwa hana la kufanya.
Henrikh Mkhitaryan aliiandikia Manchester United bao la pili katika dakika 48.Hilo limekuwa ni bao lake la sita kwenye michuano ya Europa Ligi msimu huu.
Ushindi huo umeipa Manchester United nafasi ya kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.Pia Manchester United imekuwa timu ya tano kutwaa vikombe vyote vya Ulaya (Klabu bingwa na Europa Ligi).Timu nyingine ni Ajax, Chelsea,Juventus na Bayern Munich.
0 comments:
Post a Comment