Kigali,Rwanda.
SINGIDA UNITED imeripotiwa kuwa iko mbioni kukamilisha usajili wa beki wa kulia wa APR ya Rwanda,Michael Ruseshangoga.
Ruseshangoga anayeichezea pia timu ya taifa ya Rwanda,Amavubi ameripotiwa kuwa tayari ameshakubali kutua Singida United kwa dau la Dola 50,000 (Milioni 120)
Taarifa kutoka jijini Kigali zinasema Ruseshangoga atasaini mkataba wa miaka miwili na atakuwa akilipwa mshahara wa Dola 3,000 (Milioni 4.2) kwa mwezi.
Pia beki huyo mwenye umri wa miaka 23 atapewa nyumba (Makazi) pamoja na gari ya kutembelea.
Ikiwa usajili huo utakamilika atakuwa mchezaji wa sita kujiunga na Singida United ambayo imerejea ligi kuu msimu huu baada ya kushuka daraja miaka 16 iliyopita.
0 comments:
Post a Comment