London,England.
KIUNGO wa Chelsea Mfaransa,N'Golo Kante ameendelea kulichimbia jina lake ndani ya vitabu vya kumbukumbu baada ya leo hii kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa ligi kuu ya soka nchini England maarufu kama EA Sports Premier League Player of the Season.
Kante mwenye umri wa miaka 26 ametwaa tuzo hiyo baada ya msimu huu kuonyesha kiwango bora kabisa akiwa na Chelsea aliyojiunga nayo mwezi Agosti mwaka jana akitokea Leceister City kwa ada ya £32.5m.
Eden Hazard,Cesar,Azpilicueta,Harry Kane,Dele Alli,Jan Vertonghen,Romelu Lukaku na Alexis Sanchez ni majina mengine yaliyoingia kwenye kinyang'anyiro cha kuiwania tuzo hiyo ambayo msimu uliopita ilienda kwa Jamie vardy wa Leceister City.
Ikumbukwe Kante ndiye mshindi wa msimu huu wa tuzo za PFA na FWA.Wiki iliyopita Kante alitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa Ufaransa kwa wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment