728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 26, 2017

    Antonio Valencia alamba dili jipya Man United


    Manchester, England

    STAA wa kimataifa wa Ecuador,Antonio Valencia amelamba dili jipya la miaka miwili la kuendelea kuichezea klabu yake ya Manchester United na sasa ataendelea kuwepo kuwepo klabu hapo mpaka mwaka 2019.

    Dili hilo jipya limekuja siku moja tu imepita tangu mlinzi huyo wa kulia aiongoze Manchester United kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa michuano ya Europa Ligi baada ya kuinyuka Ajax mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa huko Friends Arena,Sweden.

    Akiwa na Manchester United,Valencia amecheza jumla ya michezo 291 akifunga mabao 22 na kupika mengine 61.Ametwaa mataji mawili ya ligi kuu,mataji mawili ya kombe la ligi,taji moja la FA na taji moja la Europa Ligi.

    Valencia mwenye umri wa miaka 31alijiunga na Manchester United mwaka 2009 akitokea Wigan kwa ada ya Pauni Milioni 17.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Antonio Valencia alamba dili jipya Man United Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top